Posts

Showing posts from June, 2020

IJUE VITA YA MCHANGA NA NGUVU ZA SAND MAFIAS

Image
Mchanga: Ni moja kati ya maliasili zinazotumika kwa wingi Duniani. Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaripoti kuwa, uchimbaji wa mchanga na kokoto unazidi Tani Bilioni 40 kwa mwaka, kwa sababu ya uhitaji mkubwa wa maliasili hiyo. Kuongezeka kwa matumizi ya maliasili ya mchanga kumesababisha ¾ ya fukwe za duniani tayari zimepunguwa kwa sababu ya ongezeko kubwa la matumizi ya mchanga (sand beach). Mchanga ni maliasili inayotumika kwenye maisha yetu ya kila siku kwa matumizi mbalimbali kama vile ujenzi wa madaraja, nyumba, viwanja vya ndege na majengo marefu na kufanya kuwa moja ya maliasili muhimu sana kwenye shughuli nzima ya ujenzi wa mwanadamu. Mchanga pia unatumika kwenye utengenezaji wa microchips za computer (tarakilishi) na smart phones (sikanu).  Katika sekta inayochukua asilimia kubwa ya mchanga ni sekta ya ujenzi. Karibia nusu ya watu Duniani hivi sasa wanaishi mijini. Inakadiriwa mpaka kufikia 2030 asilimia 60 ya watu duniani kote watakuwa wanaishi mij...