IJUE VITA YA MCHANGA NA NGUVU ZA SAND MAFIAS
Mchanga: Ni moja kati ya maliasili
zinazotumika kwa wingi Duniani. Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaripoti
kuwa, uchimbaji wa mchanga na kokoto unazidi Tani Bilioni 40 kwa mwaka,
kwa sababu ya uhitaji mkubwa wa maliasili hiyo. Kuongezeka kwa matumizi
ya maliasili ya mchanga kumesababisha ¾ ya fukwe za duniani tayari
zimepunguwa kwa sababu ya ongezeko kubwa la matumizi ya mchanga (sand
beach).
Mchanga ni maliasili inayotumika kwenye maisha yetu ya kila siku kwa
matumizi mbalimbali kama vile ujenzi wa madaraja, nyumba, viwanja vya
ndege na majengo marefu na kufanya kuwa moja ya maliasili muhimu sana
kwenye shughuli nzima ya ujenzi wa mwanadamu. Mchanga pia unatumika
kwenye utengenezaji wa microchips za computer (tarakilishi) na smart
phones (sikanu).
Katika sekta inayochukua asilimia kubwa ya mchanga ni sekta ya ujenzi.
Karibia nusu ya watu Duniani hivi sasa wanaishi mijini. Inakadiriwa
mpaka kufikia 2030 asilimia 60 ya watu duniani kote watakuwa wanaishi
mijini. Ujenzi wa miji na kupanaku kwa miji mikubwa duniani inahitaji
concrete na Asphalt zote zinatengenezwa kwa kutumia Mchanga.
“Ni sawa na hewa tunayoivuta, huwa atuifikiri sana, lakini hatuwezi kuishi bila ya Hewa,”
alisema Kiran Pereira (THE FOUNDER OF SAND STORIES). Katika maeneo
mengi ya dunia mchanga umekuwa hadimu na kusababisha kuibuka kwa vikundi
vya watu kama vile smuggling Bands or Sand Mafias. Watu wanaongoza na
kumiliki kikundi cha Sand Mafias ndio hao hao wanaomiliki biashara kubwa
za nyenzo za ujenzi (Construction Material Businesses) na majengo
marefu huko Bombay nchini India. Sand Mafias mikono yao imepenya mpaka
kwenye serikali ya nchi hiyo ni kikundi cha watu wenye fedha na network
kubwa serikalini. Lakini Jarida la Times of India liliripoti kuwa
illegal sand mining ina thamani ya dola 2.3 Bilioni kwa mwaka, kwa eneo
la Tamil Nadu peke yake tu.
Mchanga ni kati ya rasilimali
ambazo zipo kwa wingi sana Duniani lakini uchimbwa kwa kasi kubwa sana
kuliko kiwango chake cha kujitengeneza upya (Natural Renewal Rate).
Duniani kote, biashara ya uchimbaji mchanga inayotambulika kisheria ina
thamani ya dola 70 Bilioni sawa na GDP (Gross Domestic Product) ya nchi
ya kenya.
NOTE: GROSS DOMESTIC PRODUCT – The Total value of goods produced and services provided in a country during one year.
Singapore ni mfano mzuri wa nchi zenye matumizi makubwa ya mchanga, kati
ya mwaka 1990 mpaka 2017 idadi ya watu walioongezeka mijini ni mara
mbili kutoka 3 milioni mpaka 5.6 milioni. Eneo la miji limekuwa kutokana
na kufanyiwa Land Reclamation kutoka 581.5 square km kati ya mwaka 1960
na kufikia 719.7 square km hivi sasa. Reclaiming kilomita moja ya mraba
ya ardhi kutoka kwenye bahari inagharimu karibu 37.5 milioni cubic
metres za mchanga.
Katika mwaka 2016 Singapore imeagiza 35 milioni metric tonnes za mchanga
kutoka Cambodia. Pia katika mwezi Julai 2017, Cambodia wakazuia mauzo
yote ya mchanga kwenda katika nchi ya Singapore. Huku Malaysia,
Indonesia na Vietnam tayari wameweka vikwazo kwenye biashara ya mchanga
kwenda Singapore, kutokana na vikwazo vilivyowekwa vimepelekea kuibuka
na kushamiri kwa biashara ya magendo ya uchimbaji na uzaji wa maliasili
ya mchanga.
THE WORLD IS ONLY SLOWLY WAKING UP TO THE FACT THAT ANOTHER FINITE RESOURCE IS SLIPPING THROUGH OUR FINGERS.
#SANDWARS
Comments
Post a Comment