MTO KONGO (CONGO RIVER) NA SIFA ZAKE

MTO KONGO (CONGO RIVER) NA SIFA ZAKE
Afrika ni moja kati ya bara ambalo limebarikiwa sana kuwa na vivutio vya aina mbalimbali. Moja kati ya vivutio hivyo ni Mto Kongo. Mto Kongo (Congo River) ni mto wa pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya Mto Nile (Nile River), lakini pia ni mto wa tisa kwa ukubwa duniani. Vyanzo vikuu vya Mto Kongo ni Milima na Nyanda za Juu za Bonde la Ufa la Afrika Mashariki (East Africa Rift Valley), Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika) na Ziwa Mweru (ndio chanzo cha mto Lualaba).

                 

 FAHAMU SIFA ZA KIPEKEE KUHUSU MTO KONGO (CONGO RIVER)
  1. Mto wa pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya Mto Nile (Nile River).
  2. Mto wa pili duniani kwa kupeleka kiasi kikubwa cha maji baharini baada ya Mto Amazon wa Amerika ya Kusini (South America).
  3. Mto Kongo ndio mto wenye kina kirefu zaidi duniani, unakadiriwa kuwa na kina zaidi ya 230 mita.
  4. Jina la Mto limetokana na ufalme wa Kongo (Ancient Congo Kingdom) wa hapo zamani, ufalme huo ulikuwepo maeneo ya karibu kuzunguka mdomo wa mto Kongo.
  5. Mitambo ya kuzalisha nishati ya umeme (Hydroelectric plants) inakidiriwa siyo chini ya 40 ndani Mto Kongo ni mto ambao maji yake yananguvu sana kiasi kwamba unauwezo wa kutoa na kukidhi mahitaji ya umeme katika nchi zote za kusini mwa Jangwa la Sahara (Sub-Saharan Africa).
  6. Katika mwaka 1482 Diego Cao ndio alikuwa Mzungu wa kwanza kutoka Ulaya kufika na kujionea Mto Kongo.
  7. Mto Kongo unakatisha katika mstari wa Ikweta (Equator) mara mbili.
  8. Nchi mbili za Afrika majina yake yametokana na uwepo wa Mto Kongo, ambazo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo) na Jamhuri ya Kongo (The Republic of the Congo).
  9. Jina la Mto lilibadilishwa kutoka Mto Zaire na kuitwa Mto Kongo mwaka 1997 baada ya Nchi ya Zaire kubadilisha jina lake na kujiita Jamhuru ya Kidemokrasia ya Kongo (Democratic Republic of Congo). The State of Zaire (1971-1997) ilipewa jina kutokana na Mto Zaire ambao hivi sasa unaitwa Mto Kongo baada ya kubadilishwa jina mwaka 1997.
  10. Unakadiriwa kuwa na visiwa vidogo vidogo zaida ya 4000 huku 50 kati ya hivyo vinakidiriwa kuwa na ukubwa zaidi ya (miles) 10 urefu.

                          



  • Vyanzo (Sources)  ๐Ÿ‘‰ Lake Tanganyika, Lake Mweru and Highlands and Mountains of East
  • African Rift Valley. 
  • Urefu (Length)      ๐Ÿ‘‰ 4700 km
  • Bonde (Basin Cover)  ๐Ÿ‘‰ 4,014,500 km square.
  • Mdomo wa Mto (River Mouth) ๐Ÿ‘‰ Atlantic Ocean

REFERENCES
https://en.wikipedia.org/wiki/Congo_River.  Retrieved on 2018-07-05. 
https://www.britannica.com/place/Congo-River
https://answersafrica.com/all-there-is-to-know-about-the-congo-river.html
https://africa-facts.org/congo-river-fun-facts/
https://interesting-africa-facts.com/Africa-Landforms/Congo-River-Facts.html
https://www.nationalgeographic.com/magazine/2015/10/congo-river-central-africas-water-highway/
Dickman, Kyle (2009). "Evolution in the Deepest River in the World". Science & Nature. Smithsonian Magazin.   Retrieved on 2018-07-06.


Article by John Kileo
Email:johnkileo@outlook.com
Instagram Account: joba_loxodonta77 

                       





















Comments

Popular posts from this blog

CHURA WA KIHANSI NA SAFARI YA MAREKANI

MANGROVE TREES "(MIKOKO)"