CHURA WA KIHANSI NA SAFARI YA MAREKANI

KIHANSI SPRAY TOADS
  • Taxonomy 

👉Kingdom⟹ Animalia
👉Phylum  ⟹ Chordata
👉Class      ⟹ Amphibia
👉Order     ⟹ Anura
👉Family   ⟹ Bufonidae

Vyura wa kihansi kwa jina la kisayansi wanajulikana kama "Nectophrynoides asperginis" ni aina ya vyura wa dogo ambao wanapitikana Tanzania tu, katika mkoa wa Iringa kwenye bonde la mto Kihansi na chakula chao ni wadudu (insectivorus).

IUCN (International Union For Conservation of Nature) walifanya utafiti na kugundua kuwa vyura wa kihansi wapo kwenye hatari kubwa ya kutoweka (Extinct in the wild). Awali uharibifu wa makazi yao ya asili uliotokana na utengenezaji wa bwawa la Kihansi kwa ajili ya kuzalisha umeme ulionza mwaka 1995 na kukamilika mwaka 2000 na kupelekea kupungua kwa kiasi kikubwa cha maji kwa asilimia 90 ambacho kilikua kinatiririka kutoka kwenye maporomoka ya bonde la mto kihansi. Lakini taarifa nyingine za waatalamu zinataja kuwa sababu za kutoweka kwao huenda zilisababishwa na utumiaji wa mbolea za kikemikali (artificial fertilizer) katika vyanzo vya maji yanayotiririka katika mto huo. Huku pia huwepo wa aina fulani ya fungus wanaojulikana kama chytrid. Hata hivyo mradi huo wa umeme ulisababisha uharibufu wa makazi yao ya asili na kusababisha kukosekana kwa unyevu nyevu wa kutosha na kupungua kwa mimea katika bonde hilo.

Matokeo ya uchunguzi wa IUCN kwa kutumia miongozo ya "IUCN RED LIST CATEGORIES AND CRITERIA":-
       2004→ Critically Endangered (CR)
       2006→ Critically Endangered (CR)
       2009→ Extinct in the wild (EW)
             
                                  
                                 

Vyura wa kihansi kutokana na uharibifu wa makazi yao ya asili. Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wengine wa mazingira kama vile World Conservation Society na Benki kuu ya Dunia walianzisha project ambapo takribani vyura 500 walichukuliwa na kupelekwa Marekani kwa ajili ya kuhifadhiwa na kuongeza idadi yao hili kuzuia athari ya kutoweka duniani, waligawanywa na kuhifadhiwa katika Zoo sita huko Marekani. Bronx Zoo na Toledo Zoo ndizo ambazo ziliweza kuwahifadhi na kufanikiwa kuongeza idadi yao. Maonyesho ya kwanza ya Vyura wa Kihansi nchini Marekani yalifanyika katika Toledo zoo mwaka 2005. August mwaka 2010 kundi kubwa la vyura wa kihansi walisafirishwa kutoka Bronx Zoo na Toledo Zoo mpaka Tanzania na kuhifadhiwa katika chuo kikuu cha Dar-es-salaam kwa ajili ya uzalishaji na kuongeza idadi yao kabla ya kurudishwa katika makazi yao ya asili.

Tishio la Maisha yao (Major Threats); Sababu kubwa la kupungua kwa idadi yao ilitokana na utengenezaji wa bwawa la umeme la kihansi (Kihansi Hydropower project) ambalo lilikuwa linachukua asilimia 90 ya maji yaliyokuwa yanaenda kwenye njia yake ya asili (original water flow) na kusababisha kupungua kwa kiasi kikubwa cha maji katika mto kihansi, mimea na unyevu nyevu.
                                   
                                
                                     
1. Je, wewe kama mdau wa mazingira na maliasili za nchi ya yako, je kulikuwa kuna ulazima wa vyura hawa kusafirishwa na kupelekwa nchini Marekani na wakati Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam kulikuwa na maabara ambayo ingeweza kuongeza idadi yao kama walivyofanikiwa kuongeza idadi hiyo na kuwarudisha katika makazi yao ya asili?
2. Na bado tunaendelea kusema ni vyura pekee wanaopatikana Tanzania tu, kama nilivyotype mwanzoni mwa uzi huu. Kama waligawanywa katika Zoo 6 nchini Marekani na Zoo 2 tu kati ya hizo 6 ndizo zilifanikiwa kuongeza idadi yao. Kwa nini hizo zoo 4 zilizobaki walishindwa kuongeza idadi yao maradufu?
3. Je, wasomi wetu wa wildlife management wa SUA, MWEKA na UDSM walishindwa wapi kuhusiana na uhifadhi na uzalishaji wa vyura hawa na kupelekea kusafirishwa mpaka nchini Marekani?
4. Je, kama ni issue ya teknolojia na vifaa vya uhifadhi na uzalishaji wa vyura hao, walishindwa kuviinstall hapa hapa katika maabara zetu na kupunguza usumbufu na gharama za usafirishaji wa vyura hao?

Namalizia kwa kusema kwamba Wazungu sio wajinga hata kidogo.


Article by John Kileo
Email:johnkileo@outlook.com

                       

                                      



Comments

Popular posts from this blog

MTO KONGO (CONGO RIVER) NA SIFA ZAKE

MANGROVE TREES "(MIKOKO)"