VETIVER GRASS
VETIVER GRASS Vetiver Grass ni aina ya nyasi ndefu ambazo majani yake ni marefu, membamba na magumu. Vetiver Grass kwa jina la kisayansi zinajulikana kama " Chrysopogon zizanioides " na asili yake ni India. Vetiver Grass zinauwezo wa kukua mpaka sentimita 150 ambazo ni sawa na futi tano na mizizi yake inauwezo wa kwenda chini mita 2 mpaka mita 4 chini ya udongo. Mizizi yake ni membamba na imara na haina stolons wala rhizomes, Vetiver roots (mizizi) inauwezo wa kuvumilia ukame na kuzuia mmomonyoko wa udongo. Nchi zinazoongoza katika uzalishaji wa vetiver grass ni Haiti, India na Indonesia. FAIDA ZA VETIVER GRASS KATIKA MAZINGIRA Utumika kwenye kuwezeka nyumba za nyasi. Ni chakula cha mifugo na pia inatumika kama ladha (flavor) katika vinywaji vya maziwa kama vile (milkshakes) na (ice creams). Kama mimea mingine inahifadhi carbondioxide kutoka angani na kutoa oksijeni katika kitendo cha mmea kujitengenezea chakula chake kijulikanacho kama "Ph