VETIVER GRASS

VETIVER GRASS 

Vetiver Grass ni aina ya nyasi ndefu ambazo majani yake ni marefu, membamba na magumu. Vetiver Grass kwa jina la kisayansi zinajulikana kama "Chrysopogon zizanioides" na asili yake ni India.

Vetiver Grass zinauwezo wa kukua mpaka sentimita 150 ambazo ni sawa na futi tano na mizizi yake inauwezo wa kwenda chini mita 2 mpaka mita 4 chini ya udongo. Mizizi yake ni membamba na imara na haina stolons wala rhizomes, Vetiver roots (mizizi) inauwezo wa kuvumilia ukame na kuzuia mmomonyoko wa udongo. Nchi zinazoongoza katika uzalishaji wa vetiver grass ni Haiti, India na Indonesia.
              
FAIDA ZA VETIVER GRASS KATIKA MAZINGIRA
  • Utumika kwenye kuwezeka nyumba za nyasi.
  • Ni chakula cha mifugo na pia inatumika kama ladha (flavor) katika vinywaji vya maziwa kama vile (milkshakes) na (ice creams).
  • Kama mimea mingine inahifadhi carbondioxide kutoka angani na kutoa oksijeni katika kitendo cha mmea kujitengenezea chakula chake kijulikanacho kama "Photosynthesis".
  • Mizizi yake huondoa nitrates, phosphates and heavy metals contaminants katika udongo.
  • Inauwezo mkubwa wa kuzuia mmomonyoko wa udongo, kulinda na kuzuia maji ya ardhini (Ground water) kutokauka kutokana na shughuli za mwanadamu na mabadiliko ya tabia ya nchi.
  • Pia inauwezo mkubwa wa kuvumiliana na udongo wenye "high and low pH", chumvi (salinity) na madini chuma (Heavy metal).
  • Miaka ya karibuni vetiver grasses zimekua zikitumika kwenye uzalishaji wa manukato (perfume), sabuni (soap) na creams.
  • Vetiver grasses zinauwezo wa kuondoa mafuta katika udongo (fuel-contaminated soil) na kufanya udongo kuwa safi tena (fuel free).
  • Vetiver grasses zimekua zikitumika kama dawa ya kienyeji (traditional medicine) kwa baadhi ya jamii za nchi kama India, Pakistan, Sri-Lanka, Malaysia, Indonesia, Thailand na jamii za West Africa.

NB: Moja ya tatizo kubwa ambalo nchi nyingi duniani kama Tanzania na Kenya zinajitahidi kupambana nalo na kulitafutia ufumbuzi ni mmomonyoko wa udongo ambapo tani kwa tani za udongo hupotea kila mwaka duniani kwa sababu ya mmomonyoko wa udongo. Upandaji wa vetiver grasses katika maeneo yaliyoathiriwa na mmomonyoko wa udongo na pia katika miteremko mikali ya ardhi (slope) husaidia kuzuia kwa kiasi kikubwa kasi ya kuondelewa kwa tabaka la juu la udongo. Moja ya njia salama kwa mazingira ambayo utumiwa sehemu nyingi duniani kupambana na mmomonyoko wa udongo ni utumiaji wa vetiver grasses. Tanzania katika mgodi wa Bulyanhulu Gold Mine Limited (BGML) ukiongozwa na Environmental Rehabilitation Officer "Digna Isdory" wanatumia vetiver grasses katika swala zima la kupambana na janga la mmomonyoko wa udongo (soil erosion) katika maeneo mbalimbali ya mgodi huo.
                 

  • Article by John Kileo
  • Email:johnkileo@outlook.com                       



                                       

Comments

Popular posts from this blog

MTO KONGO (CONGO RIVER) NA SIFA ZAKE

CHURA WA KIHANSI NA SAFARI YA MAREKANI

MANGROVE TREES "(MIKOKO)"