ULIMWENGU WA PLASTIKI AU DUNIA YA WATU



Plastiki ni polymers. Plastiki utengenezwa kwa kiasi kikubwa na material aina ya organic polymers. Polyethylene na nylon ni mfano mzuri wa organic polymers. Kauli mbiu ya mazingira mwaka 2018 duniani kote ni "Kupiga vita uchafuzi wa plastiki" (Beat Plastic Pollution)Kilele cha kuadhimisha siku hiyo ya mazingira kilifanyika nchini India. Huku kauli mbiu ya mazingira mwaka 2018 kwa Tanzania ni "Nitunze Nikutunze" ikilenga kusisitiza utumiaji wa nishati mbadala na watu kuachana na matumizi ya mkaa.

Note: Polymer is a substance made of many repeating units. The word polymer comes from two Greek words: Poly, meaning 'many' and meros meaning 'parts' or 'units'.

Kwa nini Plastiki? (Tuangalie Historia): Watafiti wanasema kuanzia mwaka 1950 mpaka 1970 asilimia ndogo sana ya plastiki ilikuwa ikizalishwa duniani kote. Kwa sababu hiyo waliweza kusimamia vizuri na kuzuia madhara yatokanayo na plastiki katika mazingira asilia. Lakini kuanzia mwaka 1990 mpaka hivi sasa, uchafu wa plastiki ambao umezalishwa ni mara tatu ya miongo miwili kutoka mwaka 1950 mpaka 1960 na kutoka 1960 mpaka 1970.
Watafiti (Researchers) wamekadiria kwamba  zaidi ya tani bilioni 8.3 za plastiki zimezalishwa kuanzia mwaka 1950 mpaka sasa. Asilimia 60 kati ya hizo zimeishia katika mazingira asilia (natural environment). Pia kuanzia  mwaka 1950 mpaka hivi sasa kiwango cha uzalishaji wa plastiki (rate of plastic production) umekuwa kwa haraka sana hapa duniani.

                    

Uchafu wa plastiki kwa sasa umezagaa karibu kila sehemu ya dunia. Wanasayansi wanaamini kuwa ni zama za mwanadamu (Anthropocene era) na matokeo ya kuongezeka kwa shughuli za mwanadamu katika dunia. Kwa sasa mwanadamu anazalisha tani milioni 300 za  uchafu wa plastiki kila mwaka duniani, inakadiriwa kukaribiana na idadi ya uzito wa watu duniani. Chupa za plastiki milioni 1 ununuliwa kila baada ya dakika moja duniani. Huku mifuko ya plastiki trilioni 5 utumika mara moja tu kabla ya kutupwa kila mwaka (single-use plastic bags). Huku nusu ya plastiki zote zinazotengenezwa duniani zinatengenezwa kwa madhumuni ya kutumika mara moja tu (single-use plastic). Ni Asilimia 9 tu ya uchafu wa plastiki ambao unazalishwa unakuwa recycled. Huku asilimia 12 uchomwa na moto, wakati asilimia 79 kati ya hizo ubakia katika mazingira yetu ya asili.
                   
Mito 10 inayobeba zaidi ya asilimia 90 ya uchafu wa plastiki ambao unaishia baharini.
1. Chang Jiang (Yangtze River) 1,469,481 tani
2. Indus 164,332 tani
3. Huang He (Yellow River) 124,249 tani
4. Hai He 91,858 tani
5. Nile 84,792 tani
6. Meghna, Brahmaputra, Ganges 72,845 tani
7. Zhujiang (Pearl River) 52,958 tani
8. Amur 38,267 tani
9. Niger 35,196 tani
10. Mekong 33,431 tani
                 
Source: Data from “Export of Plastic Debris by Rivers into the Sea” by Christian Schmidt, Tobias Krauth, and Stephan Wagner, published in Environmental Science & Technology (2017)

Mito ubeba asilimia kubwa ya uchafu wa plastiki kutoka kwenye mazingira ya mwanadamu na kupeleka baharini na kusababisha, uchafuzi wa bahari (Ocean Pollution).

Hizi ndizo nchi zinazoongoza kwa kuzalisha kiasi kikubwa cha uchafu wa plastiki ambao mwisho wake huishia baharini na kuleta madhara katika ikolojia ya bahari, China, Indonesia, Philippines, Thailand na Vietnam.

Madhara ya Uchafu wa Plastiki katika Mazingira ya Viumbe hai ; Uchafu wa plastiki una madhara sana kwa viumbe hai wa majini wakubwa na wadogo. Sumu ipatikanayo kwenye uchafu plastiki uwadhuru viumbe hai hao kama vile plankton. Lakini usababisha kifo kwa samaki wakubwa kwa kumeza kimakosa wakijiua ni chakula. kwa mfano kasa.
                     
Uchafu wa plastiki unapochomwa kama utavuta moshi wake kwa muda mrefu au mara kwa mara, basi sumu yake inaweza kukusababishia madhara makubwa katika mfumo wa upumuaji.
                   
NOTE: Most plastic items never fully disappear; they just get smaller and smaller. Many of these tiny plastic particles are swallowed by farm animals or fish who mistake them for food, and thus can find their way onto our dinner plates. They’ve also been found in a majority of the world’s tap water.

Njia mbadala za kupunguza na kuzuia uchafuzi wa plastiki.
๐Ÿ‘‰ Kutoa elimu na athari za uchafu wa plastiki kwa mazingira.
๐Ÿ‘‰ Kuweka motisha na njia nzuri za kurecycle uchafu wa plastiki.
๐Ÿ‘‰ Kuweka faini na sheria za kuzuia aina za bidhaa za plastiki ambazo hutumika mara moja tu na zinamadhara makubwa katika mazingira yetu, mfano mzuri mifuko ya nylon na chupa za plastiki
๐Ÿ‘‰ Kuweka sera ya mazingira ambayo itawabana watengenezaji na watumiaji wa bidhaa za plastiki ambao watakiuka maadili ya utupaji, utengenezaji na uhifadhi wa taka za plastiki.
                  
REFERENCES
Christian Schmidt, Tobias Krauth, and Stephan Wagner. (2017). Export of Plastic Debris by Rivers into the Sea. Published in Environmental Science & Technology.
https://www.eartheclipse.com/environment/environmental-effects-plastic-pollution.html

Article by John Kileo

Email:johnkileo@outlook.com
                       



  
          

Comments

Popular posts from this blog

MTO KONGO (CONGO RIVER) NA SIFA ZAKE

CHURA WA KIHANSI NA SAFARI YA MAREKANI

MANGROVE TREES "(MIKOKO)"